This website collects cookies to deliver better user experience

Kuhusu Sisi

Historia ya Moreplex

Hakuna siri kwamba kiwanda cha filamu kinahitaji utofauti. Kwa muda sasa, jambo hili limekua na mzozo, nakupelekea watazamaji kuhitaji waongozaji, waandaaji, waigizaji uwasilishaji na Zaidi. Watazamaji walichoshwa na haya na kupelekea kuhitaji utendaji wa nguvu kwa ajili ya upana wa tangaza maudhui kwa namna ya tofauti sasa Zaidi yasiku zote.

 

Tumeona filamu hii kabla.

Kwa “filamu hii” tunamaanisha ile inayokosa utofauti na simulizi mpya zitakazozungumzwa na watu wa rangi na dini tofauti, na kupelekea uwepo wa filamu zenye mlengo unaolenga jamii chache. Mwanzilishi wetu John Okorocha ana uzoefu wa Zaidi ya miongo mitatu katika kiwanda hiki na kuona hilo pengo la utofauti unaokosekana katika filamu. Alifahamu kutofanyia kazi hilo, kutapelekea matokeo ya hatari, kufikisha uhalisia usio wa kweli na upande mwingine nikusahau kabisa jamii zingine.

 

Na kwakua kiwanda hiki kimepiga hatua kadhaa kwa miaka ya karibuni, tunadhamiria kutengeneza kiwanda ambacho kitakua duara kile kinachotoa mtizamo halisi wa ulimwengu huu.

Hili lilipelekea mwanzo wa Moreplex.

 

Kuhusu sisi

Jukwaa kubwa kwa kila mtu.

Ilianzishwa mwaka 2017, Moreplex, ikijikita los Angeles na Lagos Nigeria, ikiwa na mlengo wa kungarisha jamii za Afrika, Ulaya na Amerika.

Tunalengo la kuwasaidia wabunifu kutengeneza filamu ambazo zitawakilisha mila na desturi nyingi, kwani tunaamini hili litaongeza uelewa na umoja katika kiwanda hiki na Zaidi.

Tunaelewa kua kuna mengi hujumuishwa katika kuandaa filamu. Tunajitahidi kulipunguza hili kwakuchukua mambo yote hayo katika uzingatiaji, kuhakikisha waandaaji wanapata njia na rasilimali zote wanazohitaji kudilisha miongozo yao ya filamu kwenda kwenye vioo vya watizamaji. Kwa mfano, Timu yetu huwashawishi waandaaji kuandaa filamu kwa lugha mbalimbali, na kuongeza uwasilishaji na kuelimisha watizamaji wengine kuhusu jamii zingine na tamaduni zao. Waigizaji ni kiwango cha juu, utayarishaji ni wa ubora, na matokeo yatakayo badili kiwanda hiki kwa ujumla.

Zaidi, tunatoa usambazaji mkubwa kupitia kebo, uangaliza wa mtandaoni, televisheni za nyumbani, Usajili wa video (SVOD), Malipo ya video kwa uhitaji (TVOD), na Zaidi ya hapo. Kwa kuweka mtandao mkubwa, tunauwezo wa kufikia watizamaji ulimwenguni kote, ikijumuisha Africa wanaoangalia nyumbani au popote pale. Sasa, wamesubiri kwa muda kuona hadithi zao zinahadithiwa na watu wanaofahamu hilo kama wao pia.

Kwa namna hii, Moreplex inaamini katika kujenga uelewa, elimu, maarifa na Zaidi kwa filamu bora Zaidi.

 

 

 

 

0:00/ 0:00
Slow Fast
  • 0.5
  • 0.6
  • 0.7
  • 0.8
  • 0.9
  • 1
  • 1.1
  • 1.2
  • 1.3
  • 1.4
  • 1.5